KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Friday, May 23, 2014

MAN CITY WAFYATA MKIA KWA YAYA TOURE, SASA KUFANYA MAZUNGUMZO YA AMANI KUEPUSHA SHARI

 Jembe la kazi: Yaya Toure ametikisa kiberiti Man City kwa kudai anataka kuondoka baada ya klabu yake kushindwa kuthamini siku yake ya kuzaliwa.
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk aliibua shari kwa kusema kuwa kuna uwezekano mkubwa nyota huyo kuondoka Etihad
Toure amefunga mabao 24 katika mechi 49 alizoichezea Man City msimu uliopita na kukiwezesha kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kutwaa ubingwa.
City wameshikilia msimamo wao kuwa Toure hataondoka kwasababu bado ana miaka mitatu katika mkataba wake aliosaini miezi 12 iliyopita  na unampatia paundi laki mbili kwa wiki.

Duh ! Huwezi amini Diamond Kachomoa hii offer…..

Kama unapenda kujua yote kuhusu Diamond basi hapa ndio umefika kwani hivi karibuni jamaa alifuatwa na agent kutoka Kenya anaepeleka wasanii nchini Dubai kwa ajili kwa kupiga show lakini kitu cha ajabu mkali huyo alichomoa offer.Jamaa tayari alikua ameweka dola za kimarekani elfu kumi na tano ( $ 15, 000) za kwenda kupiga show Dubai. Mkali huyo aliendelea na msimamo wake huo bila ya kupepesa macho kwamba hapigi show hiyo kwa kiasi hicho cha dola, bila ya kusita wala kuwaza mara mbili alisimamia msimamo wake kwamba lazima dola 20 bila ya kupungua hata dola moja. Mkali huyo pamoja na kubembelezwa kila namna lakini alimtaka agent huyo akubali hela hiyo otherwise apotezee kazi hiyo. Big up Diamond kwa kujitambua katika sanaa yetu kwani kusimamia kipato ni jukumu lako na pia ni kusaidia wasanii wadogo kukua haraka.

Rich Mavoko Alivyotua Nchini Burundi Baada ya Kupata Dili Nono Huko nchini Burundi

Rich Mavoko yupo nchini Burundi ambako amepata dili na kampuni iitwayo Ikoh ya nchini humo ambayo itahusika na yeye kuwanyanyua wasanii wa huko. Mavoko amealikwa kuwapa moyo wasanii wa Burundi na pia katika mkataba huo atatumbuiza kwenye tamasha kubwa litakalofanyila December mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu inasemekana ni deal nono ambalo litampeleka Mavoko kwenye hatua nyingine. Akisita kuweka wazi mkataba huo, Mavoko: Kwa ufupi tupo kwenye maongezi ya huo mpango kuhusu wasanii wa Burundi, mambo mazuri.”
Hizi ni picha za zingine za Mavoko akiwa Burundi.






akipokelewa baada ya kutua bunjumbura


Tazama Jinsi Msanii wa Bongo Movie Jacklin Wolper Gambe Alivyojiaabisha Kwa Kutukana Matusi ya Nguoni Kwenye Post ya Msanii Linah Sanga Mpaka Kubabisha Msanii Linah Kuiromove Post Hiyo kupitia Account yake ya Instagram





 







HAKIMU ASHINDWA KUENDESHA KESI BAADA YA WAFANYAKAZI KUFANYA MAPENZI CHUMBA CHA JIRANI NA MAHAKAMA HIYO

 
Kituko kingine leo kinatoka Italia ambapo Jaji mmoja ameamua kusimamisha kesi baada ya kuona wafanyakazi wawili wa Mahakama hiyo wakifanya mapenzi kwenye chumba cha jirani wakati kesi ikiendelea.
Jaji Anna Ivaldi alishtuka na kumuomba mwendesha mashtaka anyamaze baada ya kuona tukio hilo ndani ya ofisi pembeni ya mahakama ambapo wawili hao walidhani kioo kilichoua na tinted pembeni yao kisingeweza kumpa nafasi mtu wa upande wa pili kuona kinachoendelea ndani.
Taarifa kutoka kwenye Mahakama hiyo zinaamplfy kwamba mmoja kati ya wawili hao anatambulika kuwa yuko kwenye ndoa  na hii ni kwamujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama.
Baada ya hii ishu ilibidi tu Jaji aamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka wakati mwingine muda mfupi tu baada ya wakili Sabrina Monteverde kuanza kuzungumzia kesi ya hiyo ya Mmorocco Yasin Mahmoud ambae anashtakiwa kuua jambazi katika bandari nchini Italy mwaka jana.
Mmoja kati ya waliokuwemo mahakamani amesema “wakili ndio kwanza alianza kuzungumza, jaji akasikia kelele za mahaba na alipoangalia juu na kuona miili miwili ikiwa uchi ilifanya kila mtu akatazama ambapo tuliona watu wawili wakifanya mapenzi na inaonesha walikua hawajui kama wanaonekana na wakati tunawatazama bado walikua wanaendeleza.
Kesi ilisimamishwa na wawili hao waliondoshwa eneo hilo na kupata mshtuko ambapo majina yao hayajatajwa huku mzungumzaji wa Genoa Court  akisema kesi imesimamishwa kwa muda na tukio hilo limeshashughulikiwa na haitakuwa sawa kuzungumzia zaidi.
 

Waziri ajiua baada ya kushindwa Malawi

 
Shughuli ya kuhesabu Kura Malawi
Naibu waziri wa serikali za mitaa wa Malawi amejipiga risasi na kujiua nyumbani kwake mjini Lilongwe.
Godfrey Kamanya alikuwa anayegombea kutetea kiti chake cha
ubunge katika jimbo la Nzonzi Kusini amejiua alfajiri ya leo katika mojawapo ya vyumba vya nyumba yake iliyopo Area Ten mjini Lilongwe.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali kuu ya Kamuzu mjini humo, na jeshi la polisi litatoa taarifa rasmi ya kifo hicho baada kukamilisha uchunguzi.
Haijajulikana sababu za Kamanya kujiua japokuwa ameacha barua ya maelezo ambayo polisi wataitoa baadae.
Matokeo ya kura bado hayajatangazwa rasmi katika kile kinachosemekana kuwa uchaguzi wenye ushindani mkali sana.
Afisa mkuu wa uchaguzi, amesema kuwa mfumo wa elektroniki umeharibika na maafisa wanatumia matokeo kwa njia ya barua pepe.

SOMA ALICHOKISEMA NIKI WA PILI KUHUSU KUMRUDISHA LORD EYES KUNDINI.

Msanii wa kundi na kampuni ya Weusi, Nick wa Pili ameweka wazi kuwa siku za hivi karibuni itafahamika hatima ya Lord Eyes aliyesimamishwa kutokana na kukiuka maadili na sheria za kundi.
Weusi

Nick aliweka wazi hilo alipokuwa akichat katika ukurasa wa Facebook wa EATV alisema kuhusu hatima ya msaniii Lord Eyes ambae alisimamishwa katika kundi hilo na kudai atarudishwa soon. “Lord Eyes soon atarudi weusi maana sisi kama weusi kwa pamoja ni kampuni,hivyo weusi ni mtu 5 kama memorandam ya kampuni inavyo sema,” alisema.

Weusi walimsimamisha rapper huyo

HUYU ndiye anasadikika kuwa mwanamziki mrembo kupita wote bongo fravor

HUYU NDO MENINAH-MWANAMKE MREMBO KATIKA TASNIA YA BONGO FLAVA

Thursday, May 22, 2014

Ile video ya Mb Dogg ‘bado umenuna’ ndio imetoka, itazame hapa

Ukamilifu wa video hii ambayo picha zake niliziweka hapa wiki chache zilizopita ni huu hapa japo video hii ilikamilika wiki kadhaa nyuma lakini walikua wakisubiri muda sahihi wa kuitoa,
KAMA HAUJAIONA
>>>CLICK HAPA

Diamond Kwa Hili Inabidi Ubadilike Haraka Japo Unajitahidi kwa Mengine

Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wenye neema nyingi kwa Diamond Platnumz kimataifa. Tangu aachie video ya remix ya My Number One aliomshrikisha Davido, jina la staa huyo limekuwa kubwa kiasi cha sasa kumfanya afike sehemu ambayo hakuna msanii wa Tanzania aliyewahi kufika.

Kuanzia video yake kushika namba moja kwenye vitu vikubwa vya TV kikiwemo Trace TV, kutajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika vipengele viwili na pia kutajwa kuwania tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act: Africa. “An international music superstar from Tanzania is being born right before our eyes. Hongera sana @diamondplatnumz,” alitweet January Makamba.

Ni kweli, supastaa wa kimataifa kutoka Tanzania amezaliwa mbele ya macho yetu na ni wajibu wetu kumuunga mkono katika kila hatua anayoenda. Lakini kama unamtakia mtu heri na mafanikio zaidi, si lazima kumsifia muda wote. Ni vyema kumwambia ukweli pale ambapo tunahisi anatakiwa kuparekebisha ili asonge mbele zaidi.

Jambo muhimu ambalo Diamond anatakiwa kurekebisha ni katika live performance. Naomba nikiri kuwa pamoja na kuwa shabiki mzuri wa nyimbo nyingi za Diamond, sijawahi kupenda performance zake za live. Nimeshamhudia kwa zaidi ya mara 10 akitumbuiza na zote nimekuwa nikimuona akifanya vilevile na sipati kile ambacho nakuwa nakitegemea.

Juzi alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye show ya Road to MAMA ya MTV Base iliyofanyika Club Bilicanas akiwa pamoja na Sauti Sol na kundi la Mi Casa Music. Bahati mbaya ama nzuri kwake ni kwamba kutokana na kuwa msanii mwenyeji, yeye alikuwa msanii wa mwisho kutumbuiza. Walianza Wakenya Sauti Sol ambao kwa mtu aliyekuwa pale ukumbini atakubali kuwa show yao ilishangiliwa sana

Baadaye walifuata Mi Casa Music na wao wakadhihirisha kwanini ni kundi bora la muziki wa house kwa sasa nchini Afrika Kusini kwa kupiga show kali sana.

Diamond alifuata na kama kawaida wakati anaingia alishangiliwa mno. Kama kawaida yake, aliungana na dancers wake wanne waliokuwa wakimpa support. Ilikuwa show ya kawaida iliyoboa kwa muda mfupi tu.

Ushauri wangu kwa Diamond ni kuwa asiconcentrate sana katika kucheza na kusahau kujiimarisha katika uimbaji wa live. Haoneshi ujuzi wowote wa kuziimba nyimbo zake kiustadi anapokuwa stejini. Kwakuwa hujikuta akicheza mno na hivyo kuchoka haraka, sauti yake huharibika na kusikika vibaya na huondoa kabisa ule uprofesheno wa sauti ya msanii anayependwa na mwenye hits nyingi. Kama angekuwa anaimba na vyombo live show ingekuwa inapewa jeki na muziki tofauti unaopigwa na bendi.

Atafute namna nyingine ya kiubinifu zaidi ya uimbaji wa nyimbo zake live. Asitumbuize nyimbo kama zinavyosikika kwenye CD. Kama ataendelea na performance za kutumia DJ na CD, basi atengeneze version tofauti za beats atakazotumia kuimba live. Madhara ya hiki anachokifanya sasa ataonekana kama dancer badala ya kuwa muimbaji, sifa aliyonayo Cabo Snoop.

Kelele na shangwe anazozipata akiwa anatumbuiza zisimdanganye kuwa anazikonga nyoyo za mashabiki kwa performance kali kwakuwa ukweli ni kwamba shangwe nyingi ni kwasababu nyimbo anazoimba ni hits na wengi wanazifahamu. Kwa perfomance ya aina ile kama angekuwa ni msanii asiye na jina, wengi wasingekuwa wanarespond hivyo.


Shabiki hapendi kwenda kumuona msanii ambaye nyimbo zake hutumbuiza nyimbo zake vilevile kama zinavyosikika redioni. Kwa walioshuhudia show ya P-Square November mwaka jana pale Leaders Club waliona jinsi mapacha hao walivyo wachawi wa live performance.

Pamoja na kuwa wachezaji wazuri, hawakuwa wakicheza katika kila wimbo. Muda mwingi walikuwa wakiimba nyimbo zao kwa hisia na kuinteract vizuri na watazamaji.

Kwakuwa kutajwa kwake kwenye tuzo hizo kubwa kutampa exposure zaidi na kupata show za kimataifa, alifanyie kazi hilo ili kutowapa sababu wakosoaji na kumuona kama amebebwa tu kufika hapo.

CHANZO HABARI KWANZA$BONGO 5


HAYA NDIO MAJIBU YA MUGABE NI NOOOMAAAA CHECK.......................

Baada ya kumjib ndivyo sivyo OBAMA aona haitosh

Intro ya Video ya Nitasubiri ya JUX hii hapa,Ni Bonge la Kichupa


JUX afanya yake na hua hakose, angalia kichupa cha video yake
>>>CLICK HAPA

Tuesday, May 20, 2014

HII ndio video ya ommy dimpoz inavyopasua mawimbi kimataifa................

Hii ndio video ambayo ipo on fire mpaka kuoneshwa kwenye mtv base inaitwa ndagushima icheck hapo chini
                              CLICK HAPA

DOWNLOAD vichekesho vya mkude simba hapa ...................................


huyu ndie kitale au kwa jina analotumia sasa hv ni mkude simba platinum baby na anavichekesho vyake ambavyo anatamba navyo redio mbali mbali kama ulikuwa haujavipata isikupe shida vipate hapo
    CLICK HIZO LINK KUINGIA NA KUDOWNLOADING
 1.MKUDE SIMBA MPYA
 2.MKUDE SIMBA DENGUE
 3.MKUDE SIMBA CHENJI
4.MKUDE SIMBA
5.MKUDE SIMBA NAULI
6.MKUDE SIMBA MNYAMA
7.MKUDE SIMBA JIWE LA DHAHABU
8.MKUDE SIMBA MAFURIKO
9.MKUDE SIMBA 2

Monday, May 19, 2014

MWANAMKE AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HADHARANI...KISA?!SOMA ZAIDI HAPA.

Hivi karibuni mwanamke mmoja huko Nchini Nigeria aliuawa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu kuwa anaiba watoto wa shule na kuwapeleka kusikojulikana.

Afia kaburini baada ya kunaswa na kitu akijaribu kufukua ili aibe fuvu..soma zaidi

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari ya mtu mmoja aliyekutwa amefia kaburini kwamba  alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.
Kwa mujibu wa Saturday Tribune la Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao wakiwa salama.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hili waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.
Saturday Tribune iliongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilikuwa chanzo cha kifo chake. Na kwamba polisi hawajathibisha kuwa tukio hilo linatokana na masuala ya kishirikina.
DUNIA IMESHAKWISHA

HALI HALISI MSIBA WA ADAM KUAMBIANA

Mwili wa kuambiana ukipelekwa mochwarii hospital ya muhimbili
Rais wa Bongo Movies, Steve Nyerere akiwa analia nje ya chumba cha maiti Muhimbuli.

Wasanii na waombolezaji wakilia kwa uchungu nje ya chumba cha maiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili 
                                        R.I.P ADAM KUAMBIANA

VIDEO JIONEE MAITI YA ALIEMEZA MADAWA YA KULEVYA ANAVYOFANYIWA UPASUAJI KINYAMA........


Hii video inasadikika ya ngwear ila sina uhakika ila kikubwa ni kurekebisha tabia
hivi ndivyo wanavyofanyiwa kikatili hatareeeee sana
 CLICK HAPA KUIONA

DIAMOND PLATNUMZ AKIMBIZA KURA ZA BET AWARDS 2014, MPIGIE KURA ASHINDE

Msanii Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' kwa sasa anakimbiza katika mchakato wa upigaji kura katika Tuzo za BET 2014 ambapo  anaongoza katika kundi lake akiwa na asilimia  76.39 ya kura zote akifuatiwa na Mafikizolo wenye kura asilimia 8.17. Tuzo hizo zitatolewa Juni 29 mwaka huu jijini Los Angeles, Marekani.
click hapa umpigie kula

Sunday, May 18, 2014

HIZI NDIZO MISIBA MIWILI MIKUBWA ZA WASANII NCHINI AMBAZO ZIMEPISHANA SIKU MBILI TUU....

MSIBA WA MSANII WA DANCE NCHIN

Mmoja wa waimbaji nyota wa muziki wa dansi waliowahi kutokea hapa nchini Amina Ngaluma amefariki dunia.

Muimbaji huyo alitamba na bendi za Tam Tam na Double M Sound, amefia nchini Thailand alipokuwa akiishi kikazi kwa muda mrefu
na MSIBA WA BONGO MOVIE

                                           ADAM KUAMBIANA ENZI ZA UHAI WAKE
MPUMZIKE KWA AMAN WAPENDWA TULIWAPENDA ILA MUNGU KAWAPENDA ZAID..
                                                         AMENI.................................

Picha jionee mwenyewe DIAMOND PLATINUMZ akifanya makamuzi STAGE









Baada ya Show hii Usiku wa Kuamkia Tar.17.05.2014 hapa DSM,Diamond Platnum ameondoka Alfajiri kuelekea NChini Uingereza Kufanya Show Usiku wa leo Kuamkia Tar.18.05.2014
Kwa style hii acha alale 

Haya haya Kocha wa Barcelona ajiuzulu ni baada ya Atletico Kutwaa Ubingwa Mikononi mwa Barca


Maneno yake yamwisho haya hapa chini,
Martino “I wanted to say that I have agreed with the
club to end my time as Barcelona coach."
Martino: "We did not achieve objectives club is used to, and has done year after year. We tried until the end, but met rival better than us.”
Tata: "We apologise to the fans for not reaching the expectations."
Tata: “Above all I want to thank the group of players - to talk of their great qualities as players and as people too."
Tata: "I was proud to coach this club, we admired players from outside, then inside, & will keep doing so in what will be successful future.”
Tata: “I want to congratulate Atletico Madrid for their season - they have done very well and deserve their success.”
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...