Kama unapenda kujua yote kuhusu Diamond basi hapa ndio
umefika kwani hivi karibuni jamaa alifuatwa na agent kutoka Kenya
anaepeleka wasanii nchini Dubai kwa ajili kwa kupiga show lakini kitu
cha ajabu mkali huyo alichomoa offer.Jamaa tayari alikua ameweka dola za
kimarekani elfu kumi na tano ( $ 15, 000) za kwenda kupiga show Dubai.
Mkali huyo aliendelea na msimamo wake huo bila ya kupepesa macho kwamba
hapigi show hiyo kwa kiasi hicho cha dola, bila ya kusita wala kuwaza
mara mbili alisimamia msimamo wake kwamba lazima dola 20 bila ya
kupungua hata dola moja. Mkali huyo pamoja na kubembelezwa kila namna
lakini alimtaka agent huyo akubali hela hiyo otherwise apotezee kazi
hiyo. Big up Diamond kwa kujitambua katika sanaa yetu kwani kusimamia
kipato ni jukumu lako na pia ni kusaidia wasanii wadogo kukua haraka.
No comments :
Post a Comment