KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Friday, May 23, 2014

MAN CITY WAFYATA MKIA KWA YAYA TOURE, SASA KUFANYA MAZUNGUMZO YA AMANI KUEPUSHA SHARI

 Jembe la kazi: Yaya Toure ametikisa kiberiti Man City kwa kudai anataka kuondoka baada ya klabu yake kushindwa kuthamini siku yake ya kuzaliwa.
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk aliibua shari kwa kusema kuwa kuna uwezekano mkubwa nyota huyo kuondoka Etihad
Toure amefunga mabao 24 katika mechi 49 alizoichezea Man City msimu uliopita na kukiwezesha kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kutwaa ubingwa.
City wameshikilia msimamo wao kuwa Toure hataondoka kwasababu bado ana miaka mitatu katika mkataba wake aliosaini miezi 12 iliyopita  na unampatia paundi laki mbili kwa wiki.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...