Kituko kingine leo kinatoka Italia ambapo Jaji mmoja ameamua
kusimamisha kesi baada ya kuona wafanyakazi wawili wa Mahakama hiyo
wakifanya mapenzi kwenye chumba cha jirani wakati kesi ikiendelea.
Jaji Anna Ivaldi alishtuka na kumuomba mwendesha mashtaka anyamaze
baada ya kuona tukio hilo ndani ya ofisi pembeni ya mahakama ambapo
wawili hao walidhani kioo kilichoua na tinted pembeni yao kisingeweza
kumpa nafasi mtu wa upande wa pili kuona kinachoendelea ndani.
Taarifa kutoka kwenye Mahakama hiyo zinaamplfy kwamba mmoja kati ya
wawili hao anatambulika kuwa yuko kwenye ndoa na hii ni kwamujibu wa
mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama.
Baada
ya hii ishu ilibidi tu Jaji aamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka
wakati mwingine muda mfupi tu baada ya wakili Sabrina Monteverde kuanza
kuzungumzia kesi ya hiyo ya Mmorocco Yasin Mahmoud ambae anashtakiwa
kuua jambazi katika bandari nchini Italy mwaka jana.
Mmoja kati ya waliokuwemo mahakamani amesema “wakili ndio kwanza
alianza kuzungumza, jaji akasikia kelele za mahaba na alipoangalia juu
na kuona miili miwili ikiwa uchi ilifanya kila mtu akatazama ambapo
tuliona watu wawili wakifanya mapenzi na inaonesha walikua hawajui kama
wanaonekana na wakati tunawatazama bado walikua wanaendeleza.
Kesi ilisimamishwa na wawili hao waliondoshwa eneo hilo na kupata
mshtuko ambapo majina yao hayajatajwa huku mzungumzaji wa Genoa Court
akisema kesi imesimamishwa kwa muda na tukio hilo limeshashughulikiwa na
haitakuwa sawa kuzungumzia zaidi.
No comments :
Post a Comment