Vyombo vya habari vya Nigeria
vimeripoti habari ya mtu mmoja aliyekutwa amefia kaburini kwamba
alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe
fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.
Kwa mujibu wa Saturday Tribune
la Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun
ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa
umeingia kaburini.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na
marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya
kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao
wakiwa salama.
“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope.
Wakazi wa eneo hili waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili
wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo
hilo.
Saturday Tribune iliongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la
Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa
kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilikuwa chanzo cha kifo
chake. Na kwamba polisi hawajathibisha kuwa tukio hilo linatokana na
masuala ya kishirikina.
DUNIA IMESHAKWISHA
No comments :
Post a Comment