Ni moja ya zile stori kubwa za wiki hii
duniani ambapo CNN wameripoti kwamba taji lililokuwa likishikiliwa na
kampuni ya Toyota ya Japan iliyovunja rekodi kwa miaka mingine,
limebebwa na kampuni nyingine sasa hivi.
Data za mauzo ya magari kwenye miezi
sita ya mwanzo ya mwaka 2015 zinaonyesha kwamba kampuni ya Ujerumani
Volkswagen ndio imeshika namba 1 kwa mauzo ya magari kwenye nchi
mbalimbali za dunia na kuipiku Toyota ambayo imeuza magari MILIONI 5.02
huku Volkswagen ikiuza kwa MILIONI 5.04
Pamoja na hizo takwimu, bado Toyota
inafanya vizuri kwenye soko la Afrika kutokana na magari yake kuwa imara
na yanayoweza kumudu miundombinu mibovu ya barabara Afrika lakini pia
upatikanaji wa spare na bei zake kuwa nafuu kumezidi kuwavutia Waafrika
wengi.
No comments :
Post a Comment