Beyonce,
mume wake Jay Z pamoja na dada yake Solange Knowles wamevunja ukimya kwa
kutoa tamko la pamoja kuelezea tukio la ugomvi wa kifamilia lililotokea
May 5 ndani ya lift na video yake kuvuja.
“Kama
matokeo ya kuvuja kwa video ya ‘elevator security’ kutokea Jumatatu,
Mei 5, kumekuwa na vumi mwingi kuhusu chanzo cha tukio hilo la bahati
mbaya” Walieleza katika tamko hilo kwa shirika la habari The Associated Press.
Waliendelea,“lakini
kitu cha muhimu ni kwamba familia yetu imelifanyia kazi swala hilo..Jay
na Solange kila mmoja amewajibika kwa sehemu yake kwa kile
kilichotokea. Wote wawili wameombana radhi kila mmoja na tumeendelea
kuwa familia moja. Taarifa za Solange kulewa au kuonesha tabia
isiyoeleweka jioni ile ni za uongo.”
Pamoja na kutozungumzia sababu za kilichotokea lakini walitisha kuwa wameyamaliza,
“Mwisho
wa siku kila familia huwa na matatizo na sisi hatuna tofauti na familia
zingine. Tunapendana na kubwa kuliko yote sisi ni familia. Tumeyaacha
haya yamepita na matumaini yetu kila mtu mwingine yoyote atafanya hivyo
pia.”
Video
isiyokuwa na sauti iliyovuja Jumatatu na kuwekwa TMZ ilimuonesha dada
yake Beyonce, Solange akimshambulia shemeji yake Jay Z ndani ya lift, na
baadae kuwa tukio lililozungumziwa kila pande ya dunia kama habari
kubwa.
No comments :
Post a Comment