Kwa mujibu wa gazeti la The Daily Express, Sanchez anadaiwa kununua jumba hilo la kifahari kwa kiasi cha paund million 5.9 ambalo lipo maeneo ya Georgian mansion.
Taarifa za gazeti hilo zinaeleza kwamba Sanchez ataishi katika jumba hilo kubwa na rafiki yake wa kike aitwae Laia Grassi.
Hata hivyo muandishi wa habari hizi alimtafuta mmiliki wa jumba hilo la kifahari lililopewa jina la Fawkham Manor Farm, na kufanya nae mhojiano ambapo amekiri kufanya biashara na mchezaji wa kigeni ambaye hakuwa tayari kulitaja jina lake.
Walipoulizwa majirani, walikiri kuuzwa kwa jumba hilo na baadhi yao walionyesha kuwa na uhakika wa kumfahamu mnunuzi ambaye walimtaja kuwa ni Sanchez.
Jumba hilo lina vyumba sita vya kulala, pamoja na ukumbi mkubwa wa kupumzika, uwanja wa kutua helikopta, bwawa la kuogelea, Jacuzzi, sauna, bar pamoja na pool house.
MAPICHA ZAIDI.................
No comments :
Post a Comment