KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Thursday, July 17, 2014

WADAU WAISHUTUMU NECTA NI BAADA YA MATOKEO YA FORM 6 SOMA ZAIDI.............

Kuna wadau weng ambao wametoa dukuduku zao au mawazo yao kuhusiana na matokeo ya form 6 ambayo yametoka siku si nyingi ambapo takwimu zinaonesha;-


Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

HAYA NDIO MAONI YA WADAU MBALIMBALI KUHUSU SWALA HILO 

BRN: FROM BIG RESULTS NOW TO BRAIN RECEIVE NOTHING.!

-"Unajua maana ya BIG RESULTS NOW?? Fuatilia matokeo haya ya kidato cha sita.

Division zero mwaka jana 2604, mwaka huu 612. Tofauti watu 1992, sawa na asilimia 325%.

Division one, mwaka jana 325, mwaka huu 4,365. Tofauti 4040, sawa na asilimia 1243%. Haya ni maajabu ya karne.

Walitanua ukubwa wa goli ili iwe rahisi kufunga... Kutoka zero zaidi ya 2000 mwaka jana hadi zero 600 tu mwaka huu. Kutoka div.one 300 tu mwaka jana hadi one zaidi ya 4,000 mwaka huu.

Hivi waalimu walewale wa shule zilezile zilizotoa one 300 mwaka jana ndo wametoa one 4,000 mwaka huu??

Changamoto zao zimetatuliwa? Maabara zimejengwa? Vitabu vimeongezwa? Madai ya walimu yamelipwa? Waalimu wa Kiswahili wameacha kufundisha Hesabu kutokana na ukosefu wa waalimu wa hesabu?

Kama changamoto hizo zote hazijatatuliwa mabadiliko haya ya ghafla kutoka div.one 300 hadi div.one zaidi ya 4,000 yametoka wapi? Kweli tumeamua kutanua goli tufunge kirahisi. Karibu Tanzania, hii ndiyo BRN bhana.!

Wanasema BRN means Big Results Now, mimi namwambia Waziri Kawambwa BRN, yani he should "Better Resign Now" maana watoto wetu wanapata BRN = Brain Receive Nothing.!!

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!"

"HUYU MDAU WA FACEBOOK ANAITWA  Malisa Godlisten
Akaongezea tena

"Somo la Kiswahili wamefaulu kwa 99.87%. Yaani kati ya watahiniwa 1,000 ni mmoja tu ndiye anayedhaniwa kufeli." Najiuliza hawa waliofaulu Kiswahili ndo walewale walioulizwa hatua za kuandaa Mdahalo, wakaanza na "chemsha mdahalo wako kwa dakika 5, ..... changanya na vitunguu ... weka chumvi kwa mbali...." Au hawa ni wengine??? NECTA bhana..!!

Edward Chilangwa Kalieni kiti cha walimu. Hayo maneno yote yatazima. Kuna kuwa wajanja kwa sababu ya hao waalimu. Lakini kuvuka mpaka mpaka kukosa mwanga wa kuona kazi zao NI HATARI... ina maana moja tuu... KISIENI. Kundi la walimu laweza kuwafanya watu wasije kuwa katika mamlaka serikalini. Hesabu wangapi wakiona mwelekeo mbaya tuu KWENU ....sahau JUKWAA.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...