KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Wednesday, August 28, 2013

YANGA KUIVAA COASTAL UNION YA JIJI TANGA LEO

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara itaendelea kesho katika viwanja saba tofatuti nchini huku mabingwa watetezi, washindi wa Ngao ya Hisani na vinara wa Ligi Kuu timu ya Young Africans ikishuka dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakaribisha Coastal Union wagosi wa kaya.
Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu 2013/2014 baada ya kuanza kwa ushindi wa kishindo mchezo wake wa kwanza dhidi ya wauza mitumba watoto wa mjini Ashanti United wana Titi munda kwa kuwachapa mabao 5-1 mwishoni mwa wiki.
Kikosi cha kocha mholanzi Ernie Brandts ambacho kimekamirika kila idara, kimekua kikiendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari ya Loyola kila siku asbuhi kujiandaa na mchezo huo wa kesho dhidi ya Coastal Union.
Coastal Union ambayo inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa VPL kwenye mchezo wake wa ufunguzi iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhdi ya wenyeji maafande wa JKT Oljoro mchezo uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Yanga mabingwa mara 24 wa kombe la Ligi Kuu Tanzania bara wameanza ligi kwa kishindo na kama kauli mbiu yake inavyojieleza "DAIMA MBELE NYUMA MWIKO" imejipanga kuhakiisha inashinda kila mchezo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa mapema.
Mara baada ya mazoezi ya mwisho leo asubuhi, kocha mkuu Brandts amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri na vijana wake wapo tayari kwa mapambano na kesho watashuka dimbani kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera wa kijani na njano na kuibuka na ushindi.
"Akiongelea mchezo wa kesho amesema anajua Coastal Union wana timu nzuri, wamesajili wachezaji wazuri na wana kocha mzuri lakini hiyo haitakua kikwazo kwetu cha kutuzuia kuibuka na ushindi katika mchezo huo" alisema Brandts
Aidha Brandts aliongeza kuwa msimu huu kikosi chake kimekamilika kila idara hivyo hana wasiwasi wala hofu ya kukutana na timu yoyote katika Ligi Kuu, kwani usajili uliofanya safari hii unazidi kuifanya Yanga iendelee kuwa timu bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Wachezaji wote wamefanya mazoezi kuelekea mchezo wa kesho na kwa mujibu wa daktari wa timu  Nassoro Matuzya hakuna majeruhi hata mmoja kwa sasa, wachezaji Kelvin Yondani, Athumani Idd na Rajab Zahir waliokuwa majeruhi tayari wameanza mazoezi  tangu jana na wenzao.
Uongozi unawaomba wapenzi, wanachama na washabiki wa timu ya Yanga kesho wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa Taifa kuja kuishangilia timu yao na kuwapa hamasa vijana watakapokua wanaipeperusha bendera yenye rangi za kijani na njano.
YANGA 
COASTAL UNION

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...