JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia Yusufu Njau (32),
mkazi wa kijiji cha Roo Wilayani Hai mkoani humo, kwa kosa la kuwauwa
wazazi wake ‘kikatili’ kwa kuwakata na mapanga kichwani na kisha kuchoma
moto nyumba waliyokuwa wanaishi wazazi hao.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Robert Boaz, ameiambia FikraPevu Jumatatu
Mei 12, 2014 kuwa mtuhumiwa huyo aliyefanya kitendo cha kinyama Mei 09,
2014 saa kumi na mbili za jioni nyumbani kwao, ambapo kupitia msako
ulioendeshwa na Jeshi hilo kuanzia siku ya tukio ambapo leo (Jumatatu) saa mbili asubuhi lilimkamata akiwa nyumbani kwa kaka yake Alifa Shaibu.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika
kijiji cha Roo, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,
wakiwa katika sala ya mazishi ya marehemu iliyofanyika Mei 10, 2014,
ambapo Shahidu Njau na mkewe Minei Swai, walipokutwa na mauti baada ya
kucharangwa/katwa mapanga na mtoto wao
Boaz, amesema mtuhumiwa alimuua Baba yake mzazi, Shahibu Hassan (60),
pamoja na Mama yake mzazi, Minae Mohamed (57), ambao waliozikwa
Jumamosi, Mei 10 2014 katika
makaburi ya familia kijijini hapo.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Roo, Alfani Swai, alisema mtuhumiwa huyo
alitoka kutoka alipokuwa amejificha baada ya kukumbwa na njaa kali ndipo
alipoenda nyumbani kwa kaka yake ‘Alifa Shaibu’ kwa nia ya kuomba chai.
Amesema mara baada ya mtuhumiwa huyo kufika kwa Kaka yake alipata simu
kuwa mtuhumiwa huyo yuko katika nyumba hiyo, ndipo alipowasili na
kumpeleka mtuhumiwa katika katika kituo cha Polisi Bomang’ombe.
Wananchi wateta
Mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wananchi wa kijiji hicho
walisema kwa sasa wataishi kwa amani kijiji hapo, kutokana na kuwa na
mashaka na mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisumbua kijiji hicho kwa muda
mrefu.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya usalama nchini, inaonekana kutia
shaka wananchi kufuatia mfululizo wa matukio ya watu kutekwa, kuteswa
hata kuuawa kwa ndugu wa familia moja wa watoto na baada ya mda
watuhumiwa huripotiwa kukamatwa katika maeneo mbalimbali nchini na
sheria kuelezwa inaanza kuchukua mkondo wake kwa kuanzisha upelelezi wa
matukio hayo.
No comments :
Post a Comment