Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement
kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye
mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa
na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi
mbalimbali.
Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini
makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani
ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha
Getrude kuongea kwa kusema ‘ni
furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa
vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana‘
Getrude alianza kwa kuwasalimia
waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza
kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia
nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu
ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapa chini.
Chanzo;- United Nations na Millardayo
No comments :
Post a Comment