WATU 42 wamejeruhiwa vibaya na 21 kati yao wakiwa na hali mbaya, baada
ya gari waliliokuwa wakisafiria likitokea Mtwara kwenda jijini Dar es
Salaam kupata ajali katika eneo la Mchinga mkoani Lindi.
Kwa mjibu wa shuhuda habari zinasema ajali hiyo imetokea wakati dereva
wa basi la SB (ambaye hajatambuliwa jina) alipotaka kupishana na lori na
kusababisha ajali.
Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema ajali hiyo ilitokea mida ya saa tano asubuhi
baada ya dereva wa gari hilo ambaye ni mmoja wa majeruhi kutaka
kupishana na gari jingine lilililokuwepo barabarani.
“Huyu dereva wa basi lenye namba T607 BGD alikuwa anataka kupishana na
lori lililokuwepo katika barabara hiyo ambayo ni nyembamba kidogo na
hivyo yeye ilimfanya apande tuta la mchanga lililokuwepo katika eneo
hilo na kusababisha gari kulala upande mmoja hadi kuanguka” alisema
Mzinga.
Amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine.
CHANZO TZONE
No comments :
Post a Comment