KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Thursday, July 10, 2014

HIKI NDICHO KILICHOIKUMBA NIGERIA BAADA YA KUBEZA AMRI YA FIFA


Nigeria imepigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.
Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini.
Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.
FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.
Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.
FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.
Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15)

Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.
Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil.
Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn'goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF .
Mabingwa hao wa Afrika walishindwa katika mkondo wa pili wa kombe la dunia na Ufaransa .
Hiyo ilikuwa ni mara ya tatu kwa timu hiyo kufuzu kwa mkondo wa pili baada ya kufuzu mwaka wa 1994 na 1998.
CHANZO BBC SWAHILI

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...