Bunge la Israeli, limepitisha sheria ya kuwalisha kwa lazima wafungwa ambao wanashiriki mgomo na kususia kula.
Sheria hiyo ambayo ilikubaliwa na idadi
kubwa ya wabunge, inawaruhusu mahakimu kuhakikisha kuwa wafungwa
wanalishwa kwa lazima na pia kupata matibabu kwa lazima bila ya ruhusa
ya mfungwa ili kunusuru maisha yao.
Rais wa Palestina ambao wanazuiliwa
katika magereza ya Israeli wamekuwa wakisusia chakula kama njia yao ya
kupinga kukamatwa kwao katika miaka michache iliyopita.
Nchi hiyo inahofu kuwa wafungwa hao ambao wamekataa kula chakula huenda wakafa na kusababisha fujo magerezani.
Sheria hiyo mpya imelaaniwa na chama cha
madaktari nchini Israeli, ambacho kinaamini kuwa kuwalisha wafungwa
chakula kwa nguvu ni mbinu ya mateso na ni hatari kimatibabu.
No comments :
Post a Comment