KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Sunday, July 26, 2015

Daimond Platnumz na Rais Kikwete wameshinda hizi tuzo Afrika Kusini. (African Achievers awards)

 Ni siku saba tu zimepita toka mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz ashinde tuzo ya BEST LIVE ACT kwenye tuzo zilizotolewa na MTV BASE AFRICA Durban Afrika Kusini.

Usiku wa July 25 2015 Diamond ameshinda tuzo nyingine kwenye tuzo za AFRICAN ACHIEVERS AWARDS 2015 zilizotolewa Afrika Kusini ambako pia Diamond alihudhuria.
Location kulikotolewa tuzo zenyewe Johannesburg South Africa.
Meneja wake aitwae Salam ndio alikua wa kwanza kuwafahamisha Watanzania kupitia page yake ya twitter ambapo Mtanzania mwingine aliyeshinda tuzo kwenye usiku huu ni Rais Jakaya Kikwete aliyeshinda tuzo ya Uongozi bora na ikapokelewa na Dr. Asharose Migiro huku Diamond akichukua ya Artist of the Year kwa mujibu wa Salam.
 Tuzo hizi zimekua zikitolewa kwenye mataifa mbalimbali, mwaka huu 2015 zimetolewa Johannesburg South Africa huku za mwaka 2013 zikitolewa Nairobi Kenya, za mwaka 2014 zilitolewa Accra Ghana.
Ni tuzo ambazo zimekua zikitambua michango mbalimbali ya watu mbalimbali waliofanya bidii au kuleta mabadiliko kwenye jamii yao na zimekua zikitolewa kwenye vipengele mbalimbali kama kwa kampuni za simu, Mwanamichezo wa mwaka, Mwandishi wa habari wa mwaka, Kiongozi bora wa mwaka na nyingine.







No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...