KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Thursday, June 1, 2017

Hatutaiona KRC Genk ya Mbwana SAMATA kwenye EUROPA LEAGUE



Usiku wa May 31 2017 Club ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza game yake ya mwisho ya play off ya kuwania kushiriki michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2017/18 dhidi ya KV Oostende.
KRC Genk ambao msimu uliyoisha walifanikiwa kushiriki michuano ya Europa League na kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali na kutolewa na Celta Vigo ya Hispania, hata hivyoGenk wamejikuta wakikubali kipigo cha magoli 3-1 wakiwa ugenini dhidi ya KV Oostende.
Kama Genk wangefanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo uliyochezwa katika uwanja waAlbertpark, wangekuwa wamepata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League kwa mara nyingine tena, magoli ya Joseph Akpala dakika ya 27, David Rozehnal dakika ya 32 na Andile Jali dakika ya 51 ndio yaliyoimaliza KRC Genk.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye alipata nafasi ya kuipigania timu yake kwa dakika zote 90, hakufanikiwa kufunga goli licha ya timu yao kuutawala mchezo kwa asilimia 54 kwa 46 dhidi ya wenyeji wao na waliishia kupata goli la kufutia machozi dakika ya 43 kupitia kwa Siebe Schrijvers.
CHANZO CHA HABARI MILLARD AYO

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...