KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Monday, July 14, 2014

Pele: Ni vigumu kusahau kilichoitokea Brazil 2014


Gwiji wa soka duniani Edson Arantes do Nascimento Pele, amesema katu hatosahau kilichoikuta timu yake ya taifa ya Brazil, wakati wa fainali za kombe la dunia ambazo zilifikia tamati hapo jana kwenye ardhi ya nyumbani kwao.
Pele, aliyekuwa mmoja wa mashuhuda wa mchezo wa hatua ya fainali iliyochezwa jana huko Estádio do Maracanã, mjini Rio de Janeiro amesema taifa lake limepata pigo kubwa ambalo halitoweza kusahaulika kirahisi.
Gwiji huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 73, amesema ni vigumu kuamini kama kweli Brazil imefungwa mabao saba kwa moja kisha ikapoteza mchezo uliofuata kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri, hali ambayo anaamini inaendelea kuwaumiza wananchi wa nchi hiyo iliyo ukanda wa Amerika ya kusini.
Hata hivyo Pele akakumbushia kauli aliyowahi kuitoa kabla ya fainali za kombe la dunia hazijaanza mnamo June 12 mwaka huu, kwa kusema hakuitegemea Brazil kama ingefika mbali na aliipa nafasi kubwa timu ya taifa ya Ujerumani.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...