KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Monday, July 14, 2014

KOCHA WA ARGENTINA AJIVUNIA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE...........

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Javier 'Alex' Sabella, amekipongeza kikosi chake, kwa kazi kubwa iliyoonekana usiku wa kuamkia hii leo katika mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya kombe la dunia huko ncini Brazil.

Sabella, amesema hakuna cha kujivunia zaidi ya kukipongeza kikosi chake kwa mchezo mzuri ulionekana dhidi ya Ujerumani ambao wapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kirahisi.
Babu huyo mwenye umri wa miaka 59, amesema kwa hakika machungu yapo kwa wachezaji wake kutokana na kuukosa ubingwa wa dunia, lakini kwa upande wa uchezaji soka hana shaka nalo.
Amesema huenda bahati haikuwa kwao katika mchezo huo kutokana na wachezaji wake kutengeneza nafasi nyingi ambazo huenda zingewawezesha kuibuka mabingwa, lakini haikuwa hivyo na badala yake waliadhibiwa wao katika muda wa nyongeza.
"Wachezaji wangu wana uchungu wa kukosa ubingwa, lakini hawakucheza vibaya, walifuata maelekezo niliyowapa wakati wote hivyo kwa hilo siwezi kujutia,"
"Tuna kila sababu ya kujivunia mazuri tuliyoyafanya kwa mwaka huu, na hakuna aliyetudhania kama tungefika hapa tulipofika, ilikuwa ni safari ndefu iliyokuwa na vikwao na ninashukuru tumemaliza mchezo salama japo tumefungwa." Amesema Sabella
Hata hivyo meneja huyo wa zamani wa klabu ya Estudiantes de la Plata, amekataa kuzungumzia mustakabali wake katika timu ya taifa ya Argentina, ambapo ilitangazwa mapema ataachia ngazi mara baada ya fainali za kombe la dunia kufikia tamati huko nchini Brazil.
"Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu mustakabali wangu, hilo lipo chini yangu kutokana na utashi nilionao kuanzia kwa wachezaji, watu wangu wa karibu pamoja na familia yangu." Amesema Sabella

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...