Shirikisho la soka duniani FIFA, hii leo limetangaza orodha ya
viwango vya ubora wa soka, ikiwa ni juma moja baada ya kukamilika kwa
fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 huko nchini Brazil.
Orodha hiyo ambayo hutolewa kila mwezi, imezingatia matokeo ya
michezo ya fainali za kombe la dunia, ambapo mataifa makubwa kama
Uingereza yameonekana kutupwa mbali.
Wenyeji wa fainali za kombe la dunia Brazil nao wameonekana kuanguka
kwa kiasi kikubwa, ili hali waliokuwa mabingwa wa fainali hizo mwaka
2010 Hispania wameporomoka kwa kasi ya ajabu wakitokea nafasi ya kwanza.
Mabingwa wapya wa fainali za kombe la dunia, Ujerumani wamekalia kiti
cha orodha hiyo, baada ya kuonyesha kiwango kikubwa walipokuwa nchini
Brazil, ambapo walicheza michezo saba pasina kufungwa mchezo wowote.
Ifuatayo ni orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi July mwaka 2014.
1. Ujerumani (+1)
2. Argentina (+3)
3. Uholanzi (+12)
4. Colombia (+4)
5. Ubelgiji (+6)
6. Uruguay (+1)
7. Brazil (-4)
8. Spain (-7)
9. Uswisi (-3)
10. Ufaransa (+7)
11. Ureno (-7)
12. Chile (+2)
13. Ugiriki (+1)
14. Italia (-5)
15. Marekani (-2)
16. Costa Rica (+12)
17. Croatia (+1)
18. Mexico (+2)
19. Bosnia na Herzegovina (+2)
20. Uingereza (-10)
AFRIKA MASHARIKI NA KATI
87. Uganda (-1)
95. Kenya (+13)
96. DRC (-12)
106. Tanzania (+7)
109. Rwanda (+7)
126. Burundi (+2)
No comments :
Post a Comment