Diamond Platnumz prezda wa wasafi akifanya makamuzi Kansas City siku ya Jumapili July 6, 2014 katika kukamulisha sherehe za uhuru wa Marekani onesha lake likihudhuriwa na mashabiki wa Afrika Mashariki wakiwemo wazawa kibao waliojitokeza kumuunga mkono.
Diamond Platnumz akiendelea na makamuzi ndani huku akiwa amezungukwa na mashabiki wa Kansas City na wenggine wakiwa wamesafiri kutoka majimbo ya jirani.
Mashabiki wa Diamond Platnumz wakicheza pamoja nae wakati prezda wa wasafi akiendelea kufanya makamuzi ya nguvu ndani ya Kansas City, Missouri.
Diamond Platnumz akiendelea kufanya makamuzi ya nguvu ndani ya Kansas City MO mashabiki wengine wakipata picha mbili tatu na wengine wakiwa wanarekodi video.
Prezda na madansa wake wakiendelea kulishambulia jukwaa Kansas City.
Mashabiki wa Diamond wakiwa wamechanganyikiwa Prezda mwenyewe akiendelea na makamuzi ya nguvu.
Mashabiki kama unavyoona kwenye picha wakitaka japo wamguse prezda wa wasafi kwenye show yake ya Kansas City aliyofanya siku ya Jumapili July 6, 2014 na kuhudhuriwa na mashabiki kila kona ya Missouri na Kansas na wengine wakiwa wamekuja toka majimbo mengine ya jirani
No comments :
Post a Comment