FIFA yakatalia mbali rufaa ya Suarez |
Shirikisho la soka Duniani FIFA limekatalia mbali
ombi la rufaa la mchezaji wa Uruguay Luis Suarez dhidi ya marufuku
yake ya mizi minne kwa kosa la kumng'ata Mlinzi wa Italia .
Katika barua kwa wanahabari FIFA ilisema kuwa
imekatialia mbali ombi la Shirikisho la Soka la Uruguay la kuitaka
kupunguza adhabu ya Mshambulizi huyo wa Liverpool .Hata hivyo Suarez anauhuru wa kukata rufaa katika mahakama ya rufaa ya michezo (Court of Arbitration for Sport) iwapo hataridhika na Uamuzi huo.
Mshambulizi huyo wa Liverpool alibanduliwa nje ya kombe la dunia baada ya tukio hilo la Juni tarehe 24 na sasa anaomba msamaha ili iwe rahisi kwake angalau kujifua pamoja na wachezaji wenza huko Anfield Uingereza huku akitarajia uhamisho kuelekea Uhispania katika klabu ya Barcelona .
Tukio hilo lilikuwa la tatu kwa mshambulizi huyo bora msimu uliyopita huko Uingereza.
CHANZO BBC SHWAHILI(MICHEZO)
No comments :
Post a Comment