Akiwa
amefungiwa mechi tisa za kimataifa na miezi minne kwa ujumla
kujihusisha na soka, Suarez alirejea Uruguay akiiacha timu yake imetinga
Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.
Mashabiki
walijimwaga mitaani hadi Uwanja wa Ndege kwenda kumpokea mshambuliaji
huyo wa Liverpool nchini Uruguay, huku wengine wakiwa wamevaa picha yake
kumtukuza nyota huyo.
Rais
wa Uruguay, Jose Mujica alikuwas Uwanja wa Ndege pia kumpokea, lakini
akaamua kuondoka katakana na ndege iliyokuwa inamrejesha Suarez
kuchelewa.
Shabiki akiwa ameshika bango la kuikandia FIFA kwa kumfungia Suarez
Shabiki mdogo akiwa na meno bandia mdomoni mwake Uwanja wa Ndege wa Carrasco
Watu wakiwa wamejipanga barabarani tayari kumpokea mshambuliaji huyo wa Liverpool
Barabara ya kuelekea Uwanja wa Ndege Carrasco watu wako tayari kwa mapokezi ya Suarez
Kwa
sababu ya kuchelewa, umati wa watu wapatao 1,000 uliondolewa eneo la
Uwanja wa Ndege na kuhamishiwa katika eneo la jeshi kuendelea kumsubiri
Suarez awasili.
Mapema Suarez alipigwas picha akiwa na wachezaji wenake mjini Rio wakati wanawasili hotelini.
Uruguay itamenyana na Colombia katika 16 Bora ya Kombe la Dunia mechi ya timu za Amerika Kusini tupu.
No comments :
Post a Comment