Mkali
wa muziki wa Pop Duniani, mwanadafada ‘Rihanna’ ameonyesha kuvutiwa na
utanashati wa msakata kabumbu wa timu ya taifa ya Ghana na kiungo wa
klabu ya Fc Schalke 04 ‘Kevin
– Prince Boateng baada ya
kuweka picha ya mchezaji huyo kwenye ukurasa
wake waTwitter siku ambayo Ghana ilichezea kipigo cha bao 2 -1 toka kwa
Marekani.
”Da Bae Doe! I Might Have To Be team Ghana on this one idc idc idc”
aliandika Rihanna. Hata hivyo huenda ikamuia vigumu Riri kuweza
kumnasa mwanasoka huyo kutokana na kuwa tayari kwenye mahusiano ya
kimapenzi na mrembo Melissa Satta anayetarajia kujifungua hivi karibuni.
No comments :
Post a Comment