KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Friday, February 14, 2014

Kifupi kuhusu Valentine Day


Hii ni vizuri kuifahamu mtu wangu wa nguvu wakati unasherehekea siku hii ya Valentine na yule umpendaye ni vizuri kujua maana halisi ya hii Valentine Day ambayo imeapishwa kufanyika kila mwaka February 14. Neno Valentine lilitokana na jina ‘Valentino’ huyu alikuwa Mtakatifu wa Kiroma aliyeitwa Valentino,siku ya Valentino hufahamika kama Siku ya wapendanao na wengi wanaiita ‘Valentine Day’ ni maadhimisho ambayo hufanyika kila  mwaka.
Watu wengi husherehekea siku hii kwa kuonyesha upendo,kuthaminiana pamoja na kujaliana kati ya watu wenye mahusiano mbalimbali ya karibu japo mara nyingi siku hii hutumiwa na walio kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Valentine Day,asili ya  Siku hii ni baada ya wakristo wa zamani kuteswa hadi kufa kwa ajili ya kuupenda Ukristo na Kihistoria Mtakatifu Valentino alitumika kama kiongozi wa dini kanisani katika utawala wa mfalme Claudia.
Mfalme Claudia alimkamata na kumfunga,Mtakatifu Valentino aliteswa kwa ajili ya Imani yake ya Kikristo na Kufa  February 14 Kwa ajili ya msimamo,imani yake na kufa kwa kutetea Ukristo Papa Gelasius aliitangaza February 14 kuwa siku ya Mtakatifu Valentino mwaka 496 AD.
Katika siku hii kwako mtu wangu pengine kazi hua zinakubana kiasi cha kukosa muda wa kuwasiliana mara kwa mara na ndugu wa karibu maana ni vizuri kuwakumbuka na kuonyesha kuwa unawajali na kuwapenda,kama uko nao mbali unaweza hata kuwapigia simu na kuwaeleza upendo wako kwao kama ni baba/mama hata mlezi.
Pia si vibaya kuitumia siku hii kwa kujumuika na watu wenye kukosa mahitaji muhimu au faraja kama watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu,Wagonjwa hata wazee wetu maana si lazima utoe pesa,lakini ushiriki wako kwa chakula au mavazi unaweza kuwapatia,Happy Valentine Day watu wangu wa nguvu.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...