KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Wednesday, May 3, 2017

RONALDO AWEKA REKODI MPYA 2 BAADA YA MCHEZO WA JANA 3-0 DHIDI YA A.MADRID...


Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madriddhidi ya Atletico Madrid ulichezwa usiku wa May 2 katika uwanja wa Santiago Bernabeu, ikumbukwe huu ni mchezo ambao ulikuwa unazikutanisha timu za mji moja wa Madrid nchini Hispania.



Real Madrid katika mchezo huo wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 yalifungwa na staa wao wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo dakika ya 9, 73 na 86 ya mchezo,Ronaldo baada ya kufunga hat-trick katika mchezo huo anaweka rekodi zaidi ya moja.
Kufunga kwa Ronaldo kumemfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia yaChampions League kufunga zaidi ya magoli 50 katika hatua ya mtoano, Ronaldoamekuwa mchezaji wa kwanza Champions League kufunga hat-trick mbili mfululizo katika hatua ya mtoano kwa michezo ya kufuatana alifunga na Bayern na leo dhidi ya Atletico
Ronaldo pia anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga magoli 20 katika mchezo wa Madrid Derby yaani dhidi ya wapinzani wao wa jadi Atletico wanaotokea jiji la Madrid,Real Madrid sasa wanakazi ya kutafuta sare katika mchezo wa marudiano ili waingilea fainali lakini kesho ni Juventus dhidi ya AS Monaco.
CHANZO CHA HABARI MILLARD AYO

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...