KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Sunday, April 30, 2017

Tyson atoa tamko kusuhu maombi ya Anthony Joshua Kupanda ulingoni....



Saa chache tu zimepita tangu kumalizika kwa pambano la ndondi ambapo bondia wa Uingereza Anthony Joshua ameshinda kwa KO vs Klitschko, sasa ametaka pambano dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu Tyson Fury.
Katika interview baada ya pambano vs Wladimir Klitschko wa Ukraine lililopigwa Wembley Stadium, London na kushinda kwa KO round ya 11, Joshua alimuomba Fury ambaye ni Muingereza mwenzie wazichape: “Fury, Tyson Fury, uko wapi baby? Ni hiki unachotaka kuona? Nafurahia kupigana, napenda kupigana.
“Tyson Fury, najua ulikuwa unaongea sana na unataka kurudi na kushindana – nataka kuwapa watu 90,000 nafasi ya kuangalia usiku mwingine wa boxing. Nataka kupigana na kila mtu, nafurahia hii sasa.” – Anthony Joshua.
Naye Tyson Fury baada ya kusikia tambo hizo za Joshua alimjibu kupitia account yake ya twitter akisema amekubali kupambana ambapo aliandika: “Anthony Joshua umekubaliwa. Tutaupa ulimwengu pambano kubwa katika miaka 500. Nitacheza na wewe.” – Tyson Fury.
CHANZO Millad ayo

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...