Winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa anaekipiga kwenye klabu ya
Free State Stars inayoshiriki ligi kuu ya nchini South Afrika ameanza
vibaya ligi hiyo kwa timu yake kupokea kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa
Mpumalanga Black Aces ambayo pia ni timu iliyomsajili nyota wa Yanga
Kpah Sherman.
Bhongolwethu Jayiya alifunga goli pekee lililoipa Black Aces ushindi
kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya Afrika Kusini msimu
wa 2015/2016
uliochezwa kwenye uwanja wa Goble
Park ambao ni uwanja wa nyumbani wa Free State Stars.Ngassa alianza
kwenye kikosi cha kwanza cha Free State Stars pamoja na SthembisoNgcobo
ambaye pia ni mchezaji mpya kwenye kikosi hicho huku timu yake ikipewa
nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi lakini mambo yakawa tofauti.Kikosi
cha Free State Stars kilichoanza kwenye mchezo dhidi ya Black AcesKwenye
mchezo huo Ngassa alioneshwa kadi ya njano dakika ya 54 na baadae
dakika ya 63 alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa
na Danny Venter.Free State walishindwa kupata bao mwanzoni mwa kipindi
cha kwanza wakati walipotawala mchezo kabla ya Black Aces hawajapata bao
dakika ya 24 kwa shambulizi rahisi. Lehlohonolo Nonyane aliambaa na
mpira kisha kupiga krosi iliyomkuta Jayiya ndani ya boksi la penati na
kuukwamisha mpira wavuni.Kama walivyoanza kipindi cha kwanza, Stars
walirudi kwa kasi kipindi cha pili na ilibaki kidogo Somaeb aipatie
Stars goli la kusawazisha muda mfupi baada ya kuanzakwa kipindi cha
pili.
No comments :
Post a Comment