RAISI OBAMA |
Patrick Rushing ni Meya wa Mji wa Airway Heights ambao uko Washington, jamaa alijikuta tu akimwita Obama nyani na akamwita Michelle Obama sokwe !!
Ukizungumzia
ishu ya Ubaguzi wa rangi Marekani sio kesi ndogo, lakini Meya Rushing
amesema yeye sio mbaguzi japo aliyaandika haya kwenye ukurasa wake
Facebook “Huyu mwanamke Michelle mwenye uso wa sokwe hamvutii mtu yoyote labda Obama mwenye uso wa nyani.. waangalie masikio yao, LOL” >Patrick Rushing.
Ikainuka stori ya Halmashauri ya Jiji kumtaka ajiuzulu “Nakubali
kwamba nimekosea, ila kama nikijiuzulu itaonekana kama mimi ni mbaguzi
wakati sio kweli… Huo ni utani ambao huwa tunafanya na rafiki zangu kila
mara” Meya Rushing.
Patrick Rushing |
Gazeti moja la Marekani lilitembelea ukurasa wake wa Facebook na kukuta
post zaidi ya 75 zikihusiana na ubaguzi wa rangi, Wahamiaji wanaoishi
Marekani, zipo alizomponda Hillary Clinton na pia nyingine kawaponda wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
No comments :
Post a Comment