KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Tuesday, July 7, 2015

Floyd Mayweather amenyang’anywa mkanda wake aliomshinda Manny Pacquiao

Bingwa Floyd Mayweather kaingia kwenye headlines nyingine, kila mtu anajua kwambaFloyd ndio anayeongoza kwa kulipwa vizuri kwenye list ya Wanamichezo duniani, ni kweli kashindwa kulipa dola 200,000?

Hilo ndio deni lake ambalo ilitakiwa alipie ada yake kwenye Shirikisho la Ngumi DunianiWBO, mwisho wa siku ambayo jamaa ilitakiwa afanye malipo hayo ilikuwa July 03 2015… Mpaka sasa hivi jamaa hajafanya malipo hayo na yamefanyika maamuzi magumu kumnyang’anya mkanda wake alioshinda baada ya kumpiga Emmanuel Manny Pacquiao.
Iwapo Mayweather akinyang’anywa mkanda, Timothy Bradley atakuwa ndio Bondia anayeushikilia mkanda huo.
Floyd Mayweather baada ya ushindi wake wa May 2 2015 aliwahi kusema kwamba ataachia mikanda yake yote ili mabondia wachanga wapate nafasi ya kuishindania pia.
Mayweather ambae bado anaishikilia mikanda ya ubingwa wa uzito wa kati bado anayo nafasi ya kukata rufaa kujiokoa kwenye kitanzi cha uamuzi huo kabla ya July 20 2015.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...