Jana mji wa Bagamoyo uliingia katika taharuki kubwa baada ya habari kuenea kuwa kuna marehemu kafufuka baada ya kuthibitishwa na madaktari kuwa amefariki.
Timu ya Hekaheka ilifunga safari hadi Bagamoyo na kukuta umati wa watu katika nyumba ambayo marehemu alikua akiishi ikiwa ni muda mchache baada ya mwili wake kurejea kutoka hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo ambapo ndipo alipofariki.
Majirani walidai baada ya mwili wa marehemu huyo kurudishwa nyumbani ili kuanza taratibu za mazishi walishangaa kuona bado mwili wa moto na alikua akijitingisha wakati waoshaji wakimuandaa kwa ajili ya kumzika.
Shangazi wa marehemu alisema ni kweli baada ya kumleta walishangaa mwili ukiwa wa moto na mapigo ya moyo yakifanya kazi kama kawaida licha ya madaktari kuthibitisha kuwa amefariki, na wakaamu kusimamisha shughuli za mazishi hadi kesho yake walipoona amekuwa wa baridi na tayari alishafariki.
Daktari aliyethibitisha kama marehemu amefariki alisema baada ya kumpima marehemu alikua amefariki na kuruhusu taratibu ziendelee, na alisema kuwa mwili wa marehemu kuwa wa moto inategemee na mazingira ya sehemu alipohifadhiwa.
No comments :
Post a Comment