KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Tuesday, June 30, 2015

H Baba kayaandika haya maneno baada ya kuona video mpya ya Ali Kiba.

Mwimbaji Hamis Baba aka H Baba ameyaandika haya kwenye ukurasa wake Instagram baada ya kuiona video mpya ya Ali Kiba ‘Chekecha’ iliyochezwa kwa mara ya kwanza June 29 2015 kwenye TV ya Ufaransa ambayo kwa sasa ina umaarufu mkubwa Afrika, TraceTV

Aliandika hivi >>> ‘KIUKWELI WEE JAMAA UMENIFURAHISHA SANA KWENYE HII VIDEO, KAMA NILIOTA VILE UMEITENDEA HAKI WIMBO HUU WA CHEKETUA PIA UMECHEZA VIZURI SANA NAUFUNDI WASAUTI SASA NIMENJOY SANA KUITAZAMA NARUDIA RUDIA TUU SALUTE KIBA’
‘NAONGEA KAMA MWANAMUZIKI MWENZAKO salute KINGKIBA HUU WIMBO UMEUTENDEA HAKI SANA VIDEO HATARIIII NILICHOPENDA KWENYE HII VIDEO LOCATION ZAKE TAMU SANA UTAZANI SIO MAREKANI KAMA KINO AU MIGO’
UVAAJI ULIOVAA UNAENDANA NA CHEKETUA LILE BEAT LAKO NANGUO NIMEPENDA UNAJUA NINI UNAFANYA HONGERA ZAKO WAHUSIKA WALIOMO NDANI YA VIDEO KIAFRIKA ZAIDI HONGERAA SAAAANA
Kwa kumalizia H Baba akaandika >>> ‘Sina team yoyote humu ndani ila Kiba anajua tuache masihara, Mwanamuziki kumkubali mwenzio inaruhusiwa sio kifungo cha miaka 30 jela kama wenzangu wanavyoogopa, hii video ni kali, wimbo mkali’

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...