Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars),
Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo wa
kimataifa wa kirafiki dhidi ya Morocco utakaochezwa Septemba 5 mwaka huu
nchini Morocco.
Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini
Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari
Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Azam), Aggrey
Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar),
Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said
Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva
(Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe,
DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio 9ZESCO, Zambia).
Timu hiyo itaingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia jijini Dar es salaam.
No comments :
Post a Comment