KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Thursday, July 24, 2014

NDEGE NYINGINE YADONDOKA NA KUUA WATU ZAIDI YA 40...............


Wakati ambapo bado tunaendelea kuomboleza vifo vya watu 298 waliofariki kwenye ndege ya Malaysia, ndege nyingine ya abiria ya kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imeripotiwa kudondoka na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Ndege hiyo imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura baada ya kutokea hitilafu angani.
Waziri wa usafiri wa Taiwan, Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na wengine 11 wamejeruhiwa vibaya na kwamba ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa wanne.
Ndege hiyo, ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na kunawaka moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu.
Taiwan imekuwa ikikabiriwa na hali mbaya ya hewa inayoambatana na upepo mkali na mvua zinazoletwa na kimbunga aina ya Matmo.
Hata hivyo, kitengo cha mambo ya anga cha Taiwan kimeeleza kuwa hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza kuzuia ndege kutua.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...