Thursday, July 24, 2014
Chukua hiyo: Quick Rocka ni rapper wa Bongo aliyepanda jukwaani na watu wengi zaidi na kuwalipa
Naamini umewahi kushuhudia Live Performance nyingi za wasanii wa Bongo Fleva hasa mwaka 2014/2015 waliopanda jukwaani na dancers au watu wakuonesha vitu mbalimbali ili kunogesha show.
Lakini idadi kubwa ya dancers waliowahi kupanda jukwaani kwenye show ya rapper wa Tanzania waliolipwa na kufanya mazoezi hawawezi kufikia idadi ya watu zaidi ya 40 aliowahi kupanda nao jukwaani Quick Rocka mwaka jana ambao hata hivyo walikaa jukwaani kwa muda wa sekunde 30 tu lakini alitumia gharama kuwavalisha na kulipia uwepo wao.
Rapper huyo amefunguka katika The Jump Off ya 100.5 Times Fm wakati anachangia mjadala uliouhusu kiwango cha ubora wa Live Shows za wasanii wa Tanzania kwa kuzingatia kuwa muziki wetu unaenda level za kimataifa.
“Kwa mfano mimi nilishawahi kufanya show moja mwaka jana, ni festival huwa inafanyika. Nilipanda na watu 40, wameshika moto wamevaa majoho wakati nafanya Fire Anthen. Na walikuwepo pale kwa sekunde 30 tu wakashuka wakapanda dancers wengine.” Alisema Quick Rocka.
Amesema aliamua kufanya hivyo kwa lengo la kuwafurahisha mashabiki wake ingawa aliingia gharama.
“Na watu walipenda lakini…ni kitu ambacho nilikifikiria nikakifanya, hela ikatoka lakini mwisho wa siku ni sekunde 30 lakini watu walipenda. Naweza kusema kuandaa show yote. Mimi kuvaa, madancers wengine, mazoezi tuliyofanya siku zote a week before inaweza kwenda hadi 1.2 Million kufanya hiyo kitu. Na show ilikuwa ya dakika 15 lakini niliingia gharama hiyo.” Ameeleza.
Quick amewashauri wasanii wenzake kuhakikisha wanafanya shows nzuri ili kuongeza thamani yao katika matamasha bila kujali gharama kwanza ilimradi wanazimudu.
“Nachofirikia mimi nikipresent kwa watu. Watu wakipenda kwangu ni success. Hela inaweza kufuata baadae, lakini nifanye kitu kikubwa watu wengine waige na watu wakishapenda siku nikisema nachaji milioni sita, saba…nane mtu anasema kweli Quick nikimpa hiyo hela anafanya surprises…sio kwamba unasema tu hela halafu unafika stejini uko peke yako unaimba unashuka kwa kuwa watu wanakukubali na vitu kama hivyo. Lakini inabidi tufanye Surprises na watu waenjoy.”
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment