Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini
India,huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katika kijiji cha kijiji
cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
ikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na
maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya
hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha
Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi
kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo
katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na
janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale
kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea
nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo
hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.
No comments :
Post a Comment