KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Thursday, July 10, 2014

Justin Bieber aadhibiwa kwa kukutwa na kosa la uharibifu soma zaidi..........


Mwanamuziki maarufu wa Marekani Justin Bieber amekiri kosa la kufanya uharibifu katika nyumba ya jirani yake.

Mahakama imemtaka alipe faini ya dola 80,900 na pia kufanya kazi ya jamii kwa muda wa miaka mitano.
Wapelelezi walifanya msako kwa nyumba ya Bieber huko Calabasas Carlifonia wakitafuta ushahidi uliompelekea kusababisha uharibifu huo na baada ya msako huo rafiki mmoja wa Bieber alipatikana na mihadarati na kunaswa.
Kwa mujibu wa polisi, ushahidi huo wa video ulionaswa nyumbani mwa Bieber ulionyesha Bieber akiwasalimu maswahiba wake baada ya kurusha Mayai kwa nyumba ya jirani yake na kusababisha uharibifu.
Mashtaka ya Bieber yangewekuwa mabaya zaidi iwapo uharibifu huo ungesababisha hasara inayozidi dola elfu ishirini.
Bieber atawekwa chini ya uangalizi wa polisi kwa muda wa miaka miwili na iwapo ataonyesha mabadiliko atawachwa huru.
Mahakama pia ilitoa uamuzi kuwa Bieber apate mafunzo ya kudhibiti hasira, kikamilifu. Bieber ambaye anakabiliwa na mashtaka mengine mawili ya uhalifu huko Florida na Toronto, hakufika mahakamani uamuzi huu ulipotolewa.
Mawakili wake walisema kuwa Bieber amefurahi kuwa jambo hilo limesuluhishwa na ataendelea kusonga mbele na kuwa makini katika kazi yake ya muziki.
Tangu kisa hiki Bieber alihamia Beverly Hills kutoka Calabasas.
Uchunguzi wa hapo awali uliojaribu kufuatilia tabia za Bieber haukumpata Bieber na makosa ambayo yangepelekea kumfungulia mashtaka yoyote.
Waendesha mashtaka mahakamani walikana kumfungulia mashtaka mwaka uliopita baada ya jirani yake kulalamika kuwa mwezi Novemba 2012 Bieber aliendesha gari bila kujali na kupita eneo asilopaswa.
Hayo yakijiri, Bieber pia alishtakiwa huko Miami kwa kuendesha gari akiwa mlevi na bila lessen halali. Kesi hiyo itasikilizwa baadaye mwezi huu. Aidha, katika msururu huo wa kesi, Bieber ameshtakiwa kushambulia dereva mmoja mnamo mwezi Disemba huko Toronto.
chanzo bbc swahili

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...