Kumekuwa na sintofahamu kuhusu idadi ya tuzo alizozipata Diamond
Platinumz kwenye tuzo za AFRIMMA kwa kuwa yeye na meneja wake
walitangaza kuwa wamepata tuzo zaidi ya moja huku mtandao maalum wa tuzo
hizo ukionesha kuwa alipata tuzo moja tu.
Baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam leo asubuhi, Diamond ameeleza utata uliotokea
katika tuzo.
Amesema yeye alitajwa jukwaani kuwa mshindi wa tuzo mbili ya Msanii
Bora wa kiume Afrika Mashariki na Wimbo Bora wa kushirikiana (My Number
One Remix Feat. Davido), lakini baadae yalifanyika mabadiliko na tuzo
hiyo kupewa Mafikizolo na wimbo wa Khona waliowashirikisha Uhuru.
Ameongeza kuwa hata Sheddy Clever pia alitajwa kuwa mshindi kama producer na kuoneshwa kabisa.
“Hata producer ambaye alikuwa ametangazwa ameshinda ni Sheddy
Clever kwa sababu walimuonesha mpaka anapiga kinanda, maclip yake. Kama
waliweza kuedit hata vinanda vyake anapiga yuko studio ina maanisha yeye
ndiye alikuwa ameshinda. Na wakatangaza collabo bora la kwangu mimi na
Davido. Kwa sababu tuzo hii ndiyo tulienda kupewa kwenye stage kabisa
pale. Lakini nyingine zilitangazwa kwenye TV.
“Lakini ghafla, mpaka kesho yake tukauliza mbona hatupewi tuzo
zetu mpaka sasa hivi. Kwa sababu hata dada Jide naamini anaweza kupata
leo au muda mfupi leo. Sasa baadae wakaanza kusema kuna vitu vilikosewa
sijui nini na nini…sikutaka tena kucomplain, kwa sababu nimeshapata
yangu hii sikutaka kuleta matatizo mengine.”
Hata hivyo, Diamond amesema anakubali kuwa alishinda tuzo moja na huenda kwenye kutangaza AFRIMMA walijichanganya wenyewe.
No comments :
Post a Comment