KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Friday, July 25, 2014

Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani.


Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata moja.

Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 50 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...