KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Wednesday, June 18, 2014

KIJANA AUAWA BAADA YA KUVAMIA NYUMBA NA KUMCHARANGA MAPANGA MWANAMKE


Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30) ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32)  wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya Kalangalala mjini Geita .
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo inadaiwa kuwa watu watatu akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga hodi wakidai kuwa wao na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.Baada ya Monica Lutonja kufungua 

walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kupoteza fahamu.Hata hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani kutoka na kuanza kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata mmoja na wakaanza kumpiga hadi kumuua.Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa  watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na jeshi la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...