KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Friday, August 23, 2013

NURDIN BAKARI AIBUKIA RHINO ,SASA KUKIPIGA DHIDI YA SIMBA

Kiungo wa zamani wa Simba, Nurdin Bakari amesema hawana hofu na Simba ambayo watacheza nayo kesho Jumamosi katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.



Nurdin ambaye pia aliwahi kukipiga na Yanga kabla ya kutua Rhino ya Tabora, amesema kikosi chake kiko sawa na Simba watakiona.

Nurdin alisema Simba wasitarajie mteremko kutoka kwenye timu yao kwa kuwa wachezaji wao wote wamewahi kushiriki ligi hivyo hawana hofu.

“Ugeni wetu katika ligi si tatizo sisi tumejiandaa vizuri, ninaimani tutashinda mchezo huo kwakuwa timu yetu inawachezaji wazuri ambao wamewahi kucheza ligi lakini zaidi tusubiri dakika 90,” alisema Nurdin.

Nurdin ni kati ya viungo walioachwa na Simba wakiwa katika kiwango kizuri na akatua Yanga na kufanya vema pia.

Lakini baadaye wakamuacha na sasa ametua katika timu hiyo ya jeshi ambayo imepanda ligi kuu msimu huu.
CHANZO;HABARI KWANZA

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...