Baada ya
Tanzania kufanikiwa kuchukua mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka
Uganda ambapo Bomba hilo linatarajiwa kujengwa kutoka Uganda mpaka
Bandari ya Tanga na mradi huo ukikamilika utaliingizia Taifa bil 4.8
kila siku.
Aprili 25 2016 Balozi wa China nchini Lu Youqing amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo ambapo pia amemkabidhi barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping.
Balozi Lu amethibitisha
China kuwa itashirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa
ujenzi wa reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,561 kwa kiwango cha
kisasa yaani “Standard Gauge” ambao zabuni za ujenzi zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.
Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amemweleza Balozi Lu kuwa
Tanzania imedhamiria kuanza ujenzi wa Reli ya kati haraka iwezekanavyo
na tayari imetenga fedha kiasi cha shilingi Trilioni 1 katika bajeti
yake ijayo kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi huo……..
>>>”Tuna
imani kuwa mradi huu utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya uchumi
katika nchi yetu na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na kati
zikiwemo Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio maana
hatutaki kupoteza muda kwa mazungumzo marefu, tunataka kazi ianze na
watu waanze kunufaika“:- Rais Magufuli.
Kwa upande
wake Balozi China hapa nchini Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais Magufuli
na serikali yake kwa kujiandaa kwa fedha, vifaa na rasilimali watu kwa
ajili ya kutekeleza mradi huu mkubwa na kwamba Serikali ya China,
Taasisi za fedha za China na Makampuni mbalimbali yatatoa ushirikiano
wote katika utekelezaji wa mradi huu…..
>>>”Kama
ambavyo Prof. Mbarawa amefanya mazungumzo na Serikali ya China, Taasisi
za fedha za China na Makampuni, naahidi kuwa tutaanza kazi kama ambavyo
taratibu na viwango vya ujenzi vimewekwa, tutafanya kazi kwa kujali
muda, ubora na gharama nafuu” :-Balozi Lu.
Mradi
mzima wa ujenzi wa reli ya kati unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani
Bilioni 6.8 na umepangwa kutekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza
itahusisha ujenzi wa kilometa 1,216 za kutoka Dar es salaam – Tabora –
Isaka – Mwanza na itajengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China.
Chanzo Millardayo
No comments :
Post a Comment