Kocha wa Real Madrid ya Hispania Rafael Benitez alijikuta anapata wakati mgumu kujibu swali katika mkutano na wahandishi wa habari baada ya kuulizwa kama ana amini Cristiano Ronaldo ni mchezaji bora duniani?
Ni kama Benitez alizuga kutoa jibu la swali hilo na hakutaka kabisa kumtaja Ronaldo kama mchezaji bora zaidi duniani, nafasi ambayo angepewa kocha wa zamani Carlo Ancelotti isingekuwa ishu nzito sana kwake kutoa jibu.
Kocha huyo alimtaja Ronaldo kama mmoja ya wachezaji wenye viwango vya juu kama Bale na Benzema “Ni
ngumu kusema nani ni mchezaji bora duniani, sababu kuna wachezaji wengi
wa kiwango hicho kwa muda mrefu… nafikiri Ronaldo, Bale, Benzema na
James ni wachezaji wenye viwango vya juu, na kumuweka Ronaldo miongoni
mwa wachezaji bora inatosha” Benitez
No comments :
Post a Comment