Man City VS Real Madrid July 24 2015 matokeo,Picha na Video
International Champions Cup bado inaendelea Australia kwa timu tatu kushiriki ambazo ni Manchester City kutokea Uingereza, Real Madrid ya Hispania na AS Roma ya Italia… Michuano imeandaliwa na kampuni ya Audi, ambapo July 21 2015 Man City ilicheza na AS Roma ya Italia katika uwanja wa Melbourne Cricket Ground na Man City kushinda kwa jumla kwa penati 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Cristiano Ronaldo
July 24 2015 tayari imekamilika mechi kati ya Man City na Real Madrid ya Hispania mchezo uliofanyika katika uwanja wa Melbourne Cricket Ground, mchezo umemalizika kwa Real Madrid kushinda kwa kuifunga Man City kwa jumla goli 4-1, magoli ya Madrid yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 21, Cristiano Ronaldo dakika ya 25, Pepe na Denis Cheryshev dakika ya 73 huku bao pekee la Man City likifungwa na Yaya Toure dakika ya 45.
No comments :
Post a Comment