KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Saturday, July 11, 2015

Hatimaye Ronaldinho, Eto’o na Valdes wanacheza timu moja

Kutoka kushoto ni Ronaldinho,Eto na Valdes
Wachezaji wa zamani wa Fc Barcelona ya Hispania Ronaldinho Gaucho na Victor Valdes uwenda wakaungana na mchezaji mwenzao wa zamani wa klabu hiyo Samuel Eto’o nchini Uturuki.
Story inayovutia wapenzi wa soka duniani kuhusu hawa ma star sio kucheza tena pamoja ila ni timu wanayo kwenda kuichezea Antalyaspor ya nchini Uturuki ambayo ndio imepanda daraja msimu huu. Ni nadra sana kukuta ma star wanao maliza muda wao katika soka kwenda kucheza timu inayopanda daraja na ipo katika ligi ya kawaida.
Uwenda ingekuwa kawaida kukuta ma star hawa wanacheza timu iliyopanda daraja katika ligi zinazotajwa kuwa bora zaidi duniani kama Hispania,Uingereza, Ufaransa na hata Ujerumani.
Eto’o tayari amesha saini mkataba wa miaka mitatu klabuni hapo na Ronaldinho bado ana jadili ofa hiyo licha ya kuthibitisha kupitia mitandao ya kijamii kuwa anaenda Uturuki. Lakini sasa Antalyaspor bado wanamtaka Valdes licha ya kuwa anatazamiwa na Manchester United kama mbadala wa David Degea ambae ana husishwa na kuhamia Real Madrid.
Eto’o, Valdes na Ronaldinho wamewahi kucheza Fc Barcelona katika misimu ya 2003-2004 na 2007-2008 chini ya kocha Frank Rijkard na kuisaidia klabu kutwa taji la pili la klabu bingwa barani ulaya.

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...