KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Wednesday, June 24, 2015

KUTOKA JAMII FORUM...Watanzania waonyesha kutoukubali wimbo wa Diamond Platnumz alioshirikishwa na Kcee.


Diamond Platnumz ni moja ya wasanii wanaopata collabo za kimataifa hasa za wasanii wa Nigeria na South Afrika.

 Collabo ya hivi karibuni aliyofanya Diamond Platnumz ni alioshirikishwa na Kcee, Kumekuwa na maoni tofauti ya wadau wa Muziki ambao wameonesha moja kwa moja kuwa hawaukubali wimbo huu. Haya ni Baadhi ya maoni ya watu mbalimbali katika mtandao wa Jamii Forum..
=> "Wakuu nimesikiliza tena huu wimbo mpya wa KCE feat Diamond, ni wazi kabisa huenda Dai hakujiandaa au alivamia tu collabo la watu. Ukisikiliza kwa umakini utaona kuwa, Sauti ya Dai imebanwa na haisikiki vizuri kabisa, sijui huu ndio ubanajai pua mpya au ndio unaijeria umezidi kwa huyu mzalendo wetu?
 My take: Kwa hali hii watanzania tuna haki ya kumpa kura Davido" Hayo ni maoni ya SHARDCOLE.
=> "Hilo la sauti limeshakuwa tatizo kwake sasa aliwahi haribu hata nyimbo ya Waje Coco, Pia mimi tokea aharibu kwenye ule wimbo wa Prof J siumizi tena kichwa. Huwezi kulinganisha wimbo wowote alioshiriki diamond na Kiboko Yangu ambapo King aliua vibaya sana. Hakika Ali Kiba is gifted!" haya ni maoni ya Nifah.
Yapi maoni yako


No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...