KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Monday, August 25, 2014

Video: Paka mweusi abariki ushindi wa FC Barcelona dhidi ya Elche

Wakati FC Barcelona wakianza kampeni ya kusaka ubiungwa wa nchini Hispania msimu huu, usiku wa kuamkia hii leo, hali ya taharuki ilijitokeza kwenye uwanja wa Camp Nou baada ya paka mweusi kukatiza uwanjani hapo.

Ilikuwa ni sekunde chache baada ya mchezo huo ambao ulishuhudia FC Barcelona wakicheza na Elche kuanza, ndipo paka huyo alionekana akikatiza uwanjani akitokea upande wa lango la wenyeji.
Hata hivyo hali ya taharuki ilipotea na kuwafanya wachezaji pamoja na viongozi wa timu zote mbili kuagua vicheko huku mashabiki wakishangilia kwa sauti za juu kutokana na kiumbe huyo kuingia uwanjani na kukimbia huku na kule.
Lakini yote kwa yote mmoja wa wanausalama wa uwanja wa Camp Nou alijitolea kumkimbiza paka huyo mweusi na kufanikiwa kumkamata na kumtoa nje ya eneo la kuchezea na hatimae mchezo iliendelea.
Matokeo ya mchezo huo ni kwamba FC Barcelona walichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.
CLICK HAPA KUIONA

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...