KARIBUNI KWENYE BLOG YANGU ILI USIPITWE NA HABARI KEMKEM,KWA HABARI MOTOMOTO NDANI NA NJE YA NCHI MICHEZO NA BURUDANI NA ZINGINEZO NYINGI UNGANA NAMI NICK 4REAL

Thursday, July 17, 2014

Kikosi cha Msumbiji Kutua Mchana Dar es salaam

Timu ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) inawasili Dar es Salaam kesho (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mambas itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.30 mchana kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 37 ambapo kati ya hao, 25 ni wachezaji.

Wachezaji kwenye msafara huo ni Almiro Lobo, Apson Manjate, Bone Mario Uaferro, Dario Ivan Khan, Edson Sitoe, Eduardo Jumisse, Gelicio Aurelio Banze, Helder Pelembe, Josemar Machaisse, Elias Pelembe, Isac Carvalho na Jeffrey Constatino.
Wengine ni Manuel Fernandes, Manuel Uetimane, Mario Sinamunda, Momed Hagi, Reginaldo Fait, Reinoldo Mandava, Ricardo Campos, Saddan Guambe, Simao Mate Junior, Soares Victor Soares, Stelio Ernesto, Vando Justino na Zainadine Junior.
Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Accomondia, na itaondoka Jumapili mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour.
Wakati huo huo kikosi cha Taifa Stars kimerejea jijini Dar es Salaam leo kutoka Mbeya ambapo Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kitapambana na Msumbiji (Mambas) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Benchi la Ufundi la Taifa Stars pamoja na wachezaji kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 5 asubuhi watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard iliyopo Upanga Seaview jijini Dar es Salaam.
Naye mchezaji Mwinyi Kazimoto amewasili leo 1.30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways kutoka Qatar ambapo anacheza mpira wa miguu katika klabu ya Al Markhiya ya huko. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi katika hoteli ya Protea Courtyard.
CHANZO TIMES FM

No comments :

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...