Baadhi ya walimu wanaofundisha na
waliowahi kufundisha katika shule hiyo, wameyasema hayo wakati wamepiga
simu kuomba waandishi wa habari kufuatilia zaidi mimba za utotoni kwa
wanafunzi baada ya kusoma makala isemayo mimba za utotoni tatizo Mbeya,
Pwani na Mara
Walimu nhao wamesema kuwa, kwa mwaka
mmoja katika shule hiyo si chini ya wanaunzi 10, wanaoacha masomo huku
wazazi wa wanafunzi hao wa kike na kiume wanaowapachika mimba
wakishirikiana kuzima dhambi hiyo.
Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro, aliwahi kusema kuwa wazazi watakaoshirikiana kuhusika
kuwatorosha wanaowapa mimba wanafunzi wangeweza kuchukuliwa hatua.
CHANZO;HABARI MPASUKO
CHANZO;HABARI MPASUKO
No comments :
Post a Comment