Usiku wa May 31 2017 Club ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza game yake ya mwisho ya play off ya kuwania kushiriki michuano ya UEFA Europa League msimu wa 2017/18 dhidi ya KV Oostende.
Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madriddhidi ya Atletico Madrid ulichezwa usiku wa May 2 katika uwanja wa Santiago Bernabeu, ikumbukwe huu ni mchezo ambao ulikuwa unazikutanisha timu za mji moja wa Madrid nchini Hispania.
Baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya usiku wa April 20 2016 na klabu ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya goli 2-1, sasa wanajiandaa kurudi kucheza Kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya 16.
Kwa mara ya kwanza nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Samatta akicheza dakika zote 90 na kufunga bao la uongoz kwenye timu yake ya Ubelgiji huku akiisaidia timu yake kuchomoza na ushindi wa magoli 2-1
Siku moja baada ya michezo ya robo
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuchezwa na kushuhudia vilabu kadhaa
vikiaga mashindano hayo, usiku wa April 14 ilikuwa ni zamu ya kushuhudia
robo fainali ya michuano ya UEFA Europa league.
Baada ya kumalizika kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya na kushuhudia vilabu vya Atletico Madrid, Real Madrid, Man City na FC Bayern Munich vikifuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo,
Jumatatu ya March 28 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa inajiandaa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa nne wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya Chad, habari zilizotoka March 27 kutoka shirikisho la soka Afrika CAF ni kuwa Chad wamejitoa.
Adi Yussuf ni mtanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya daraja la pili Uingereza kwenye klabu ya Mansfield Town. Adi pia amekulia katika klabu ya Leicester City ila kwa sasa yupo Tanzania kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Chad wa kuwania kufuzu michuano AFCON 2017 Gabon.
Jina la Lionel Messi sio geni duniani kote kutokana na umahiri wake na urafiki wake mkubwa na tuzo za Ballon d’Or kwa ndio mchezaji anayeongoza kwa kutwaa tuzo hizo mara tano, headlines za March 22 ni kuwa staa huyo ameamua kutanua wigo wa kipato chake.